Muungano wa mashirika ya kijamii ya Australia unaitaka serikali kuanzisha kodi ya usafirishaji ya gesi, na mageuzi ya kodi ya nyumba katika bajeti ijayo ya shirikisho. Katika taarifa ya pamoja, zaidi ya mashirika 50, ikiwa ni pamoja na Baraza la Huduma za Jamii la Australia [[ACOSS]] na Chama cha Afya ya Umma cha Australia wametoa wito wa ushuru wa usafirishaji wa gesi wa asilimia 25, mageuzi ya ushuru wa faida ya mtaji na kukomesha matumizi mabaya ya vifaa.
Mweka Hazina Jim Chalmers anasema atafanya mazungumzo na serikali za majimbo na wilaya, kuhusu kupunguza ukuaji wa Mfumo wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu. [[NDIS]]
Mfumo huo unagharimu dola bilioni 42 kwa mwaka na Bw. Chalmers anasema inakua kwa kasi sana kwa Waustralia kumudu. Ame ongezea kuwa mageuzi ya NDIS yatakuwa kipimo muhimu zaidi cha akiba katika Bajeti ya Shirikisho ya Mei 12.
Mapambano makali yameripotiwa katika jimbo la Kivu kusini kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo linalosaidiwa na Wazalendo na kundi la Twirwaneho linaloshirikiana na waasi wa AFC/M23. Kwa miongo kadhaa, jimbo la Kivu Kusini, limekuwa eneo lenye mzozo tata uliohusisha makundi yenye silaha, uasi uliopangwa, na mienendo mbalimbali yakikabila iliyokita mizizi. Miongoni mwa makundi hayo yenye silaha mna kundi la Twirwaneho ambalo kwasasa ni washirika wa waasi wa AFC/M23 wanaopigana na jeshi la Kongo ambalo pia linaungwa mkono na wanamgambo wa ndani wanaojulikana kwa jina la Wazalendo.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.




