Watch FIFA World Cup 2026™ LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari: Australia yapata usambazaji wa mafuta wa mwezi mwingine

Bench - Swahili.jpg

Serikali ya shirikisho imesema ugavi wa akiba ya mafuta ya Australia sasa umeongezwa hadi Mei, kuanzia katikati ya Aprili.


Afueni kutokana na gharama za mafuta zinazo dhoofisha imeanza kutiririka baada ya serikali ya shirikisho kupunguza kwa nusu kodi ya petroli na dizeli kwa muda, wakati serikali za majimbo pia zikikubali kuto chukua ongezeko linalotarajiwa la ushuru wa bidhaa na huduma kutokana na ongezeko kubwa la ushuru kwenye mauzo.

Marekani imesema Jumapili kuwa imemuokoa mwanajeshi wake aliyekuwa ametoweka nyuma ya uwanja wa vita tangu Iran ilipoidungua ndege ya kivita, huku Rais Donald Trump akiongeza shinikizo dhidi ya Tehran.

Nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, sasa itawapokea wahamiaji kadhaa waliofukuzwa kutoka Marekani, mpango utakotekelezwa chini ya makubaliano mapya kati ya utawala wa Kinshasa na Washington. Serikali ya Kongo inasisitiza kwamba huu si mpango wa kudumu wala utoaji wa sera ya uhamiaji ya Marekani, ambapo watu wanaohusika na mpango huu watapewa hifadhi ya muda mfupi tu.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.


Share

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now