Watch FIFA World Cup 2026™ LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari:Australia yashinikiza kupanua usitishaji mapigano Mashariki ya Kati ujumuishe Lebanon

Bench - Swahili.jpg

Waziri Mkuu Anthony Albanese ametoa wito kwa Israel kukomesha mashambulizi yake dhidi ya Lebanon, akisema usitishaji wa mapigano katika eneo hilo la Mashariki ya Kati unapaswa kupanuliwa ili kuijumuisha Lebanon.


Serikali imerudia maonyo yake kwa watumiaji kwamba unafuu wa kiuchumi kutokana na mgogoro wa mafuta hautafuata mara moja, baada ya kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.

Kikao cha kusikiliza kesi kilichopangwa kufanyika siku ya Jumatano, Aprili 8, jijini Paris, siku moja baada ya kufunguliwa kwa maadhimisho ya kila mwaka ya mauaji ya kimbari ya Watutsi nchini Rwanda, kimeahirishwa hadi Mei 6. Mahakama ya Rufaa ya Paris iliomba kuongezwa muda wa majadiliano kuhusu amri ya kuondolewa kwa kesi na kukataliwa kwa hatua za ziada za uchunguzi, ambazo zilimnufaisha Agathe Habyarimana mnamo Agosti 2025.

AC Milan, Inter Milan na Juventus wanakuja Australia kucheza michezo ya maandalizi ya msimu mpya mjini Perth. Kwa sasa Inter wanaongoza ligi ya Serie A, watakuja Australia kwa mara ya kwanza - lakini huu utakuwa mwaka wa tatu mfululizo kwa AC Milan kucheza mechi mjini Perth. Mechi ya kwanza ya Inter itakuwa debi dhidi ya AC Milan, mnamo Agosti 5; ikifuatiwa na mechi yao dhidi ya Juventus siku tatu baadaye.


Share

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now