Mbunge wa chama cha Liberal Andrew McLachlan anasema Upinzani wa Mseto haufai kutafuta mwongozo kutoka kwa chama cha One Nation kuhusu maendeleo ya sera zao, huku akiendelea kupinga pendekezo la Angus Taylor la kupunguza malipo ya ustawi wa jamii kwa watu ambao si raia.
Uchunguzi wa Seneti unaoongozwa na chama cha Greens kuhusu ukosefu wa usawa wa nyumba ulianza jana [18/5], huku chama hicho kikiwa na wasiwasi kwamba bajeti ya hivi karibuni ya serikali ya shirikisho imeshindwa kufanya chochote kwa wapangaji.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema Jumatatu itafungua vituo vitatu vya matibabu kwa ajili ya watu walioambukizwa na virusi vya Ebola katika jimbo la Ituri.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.





