Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE starting June 12 2026

Taarifa ya Habari:Chama cha Nationals chataka uchaguzi uitishwe kuhusu hatma ya mageuzi ya kodi ya serikali

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Chama cha Nationals kimemtaka Waziri Mkuu Anthony Albanese kuitisha uchaguzi mkuu, kuhusu mabadiliko hasi ya kodi ya vifaa na faida ya mtaji yaliyoainishwa katika bajeti ya shirikisho.


Published

Updated

By Gode Migerano

Presented by Gode Migerano

Source: SBS



Share this with family and friends


Chama cha Nationals kimemtaka Waziri Mkuu Anthony Albanese kuitisha uchaguzi mkuu, kuhusu mabadiliko hasi ya kodi ya vifaa na faida ya mtaji yaliyoainishwa katika bajeti ya shirikisho.


Makadirio ya Seneti yameambiwa kwamba kuongezeka kwa kasi kwa uenezaji wa itikadi kali mtandaoni sasa ni mojawapo ya changamoto muhimu zaidi zinazokabiliwa na Jeshi la Polisi la Shirikisho (AFP). Kamishna wa Polisi wa Shirikisho la Australia Krissy Barrett, anasema michakato ya uenezaji itikadi kali ambayo ilikuwa ikichukua miezi au miaka sasa inaweza kutokea ndani ya siku chache, kwa sababu vijana hasa wanalengwa kwenye majukwaa ya michezo ya kubahatisha na majukwaa mengine.

Idadi ya wanafunzi 16 wamekufa katika mkasa wa moto usiku wa kuamkia leo uliotokea katika mabweni ya shule moja ya wasichana ya Kaunti ya Nakuru nchini Kenya. Hilo ni tukio la hivi karibuni la aina hiyo kulitikisa taifa hilo la Afrika Mashariki. Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba amesema wanafunzi wengine 79 walijeruhiwa katika mkasa huo wa Shule ya Wasichana ya Utumishi, ambayo ina zaidi ya wanafunzi 800 katika eneo la Gilgil katikati mwa Kenya. Chanzo bado hakijabainika.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now