Waziri wa Nishati Chris Bowen, anasema makampuni ya mafuta yameripoti kuwa mahitaji wakati wa Pasaka yalikuwa juu kwa asilimia 30 kuliko awali.
Wana harakati wa usalama barabarani wanatoa wito wa kuteuliwa kwa waziri wa usalama barabarani wa shirikisho ili kuendesha mkakati wa kitaifa baada ya Pasaka nyingine hatari barabarani. Kufikia Jumatatu mchana 6 Aprili, angalau watu 14 walikuwa wamekufa katika ajali, huku takwimu za Australia Magharibi zikiwa bado hazijakamilika.
Nchi ya Ghana, imeungana na Msumbiji pamoja na wadau wengine kususia kongamano la nishati kuhusu bara la Afrika, linalotarajiwa kufanyika kati ya tarehe 12 hadi 14 jijini London nchini Uingereza. Kongamano hilo litakuwa muhimu na kuyaleta pamoja mataifa ya Afrika yanayozalisha nishati ya mafuta na gesi barani Afrika.
Nchini Kenya, ofisi ya rais imetangaza kujiuzulu kwa maafisa wakuu wa serikali wanaohusika na kusimamia hifadhi za mafuta. Wakati nchi hiyo, ikitegemea sana uagizaji wa mafuta kutoka nchi za Ghuba, ikitafuta vyanzo vipya vya usambazaji ili kuepuka uhaba, maafisa hawa wanashutumiwa kwa kudanganya data za hifadhi za mafuta na kupata usafirishaji wa mafuta kwa bei ya juu. Ofii ya rais unaonyesha kwamba uchunguzi unaendelea.







