Iran imethibitisha kwamba vita kati ya Marekani na Israeli katika nyanja mbalimbali Mashariki ya Kati vita isha usiku wa leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi, alizungumza kwenye runinga ya taifa ya Iran, akisema mazungumzo yatafanyika katika siku 60 zijazo, akiongeza kuwa Tehran italipiza kisasi iwapo kutatokea uvunjifu wowote wa mkataba huo. Marekani na Iran zimepangwa kusaini makubaliano ya amani nchini Uswisi Ijumaa hii 19 Juni 2026.
Kamati teule ya seneti kuhusu ukosefu wa usawa wa nyumba kati ya vizazi, imesikia kwamba Waaustralia wengi hawatawahi miliki nyumba kutokana na mfumo ambao umelenga kujenga nyumba na zana ya kuzalisha utajiri.
Uganda imekosoa vikwazo vya usafiri wa anga vilivyowekwa na nchi kama Marekani kufuatia mlipuko wa Ebola ulioenea kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikiviita "visivyo vya haki."
Afrika yasherehekea ushindi wa kwanza katika Kombe la Dunia, baada ya Ivory Coast kuibuka mshindi wa goli moja kwa sufuri dhidi ya Ecuador.






