Chama cha Greens kimeita mpango wa serikali wa kurekebisha Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Watu Wenye Ulemavu kuwa sheria 'isiyo ya kibinadamu'.
Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa
Chini ya mageuzi yaliyopendekezwa, zaidi ya watu 160,000 wataondolewa kwenye mpango huo katika jaribio la kudhibiti matumizi ya mpango huo.
Wakili mashuhuri na mwanasiasa kutoka nchini Kenya Martha Karua amezuiwa kuingia nchini Uganda na kufukuzwa nchini humo, alikokuwa amekwenda kuhudhuria kesi ya wakili Erias Lukwago aliyefunguliwa mashtaka ya uhaini. Martha Karua na Erias Lukwago ni Mawakili wa mwanasiasa mkongwe Kizza Besigye ambaye amekuwa akizuiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






