Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE starting June 12 2026

Taarifa ya Habari: Ongezeko ya bei ya mafuta yalazimisha serikali izingatie hatua zakufanyia kazi nyumbani

Bench - Swahili.jpg

Hatua za kufanyia kazi nyumbani zinaweza wasilishwa lakini mgao wa mafuta hauzingatiwi, na viongozi wanaohudhuria mkutano wa kitaifa wa baraza la mawaziri leo kuhusu mgogoro wa mafuta.


Published

Updated

By Gode Migerano

Presented by Gode Migerano

Source: SBS



Share this with family and friends


Hatua za kufanyia kazi nyumbani zinaweza wasilishwa lakini mgao wa mafuta hauzingatiwi, na viongozi wanaohudhuria mkutano wa kitaifa wa baraza la mawaziri leo kuhusu mgogoro wa mafuta.


Wakati huo huo kiongozi wa upinzani Angus Taylor amesema jambo la kwanza analotaka kuona, likitangazwa na baraza la mawaziri la kitaifa ni kupunguzwa kwa ushuru wa mafuta.

Wataalamu wa usalama wa kidijitali wanashutumu majukwaa makubwa ya teknolojia - ikiwa ni pamoja na Apple, Google na Meta na mengineyo - kwa kufumbia macho unyanyasaji ulioenea wa watoto kwenye majukwaa yao. Katika wiki iliyopita, Meta ilipatikana na hatia ya kuwadhuru watoto wanao tumia mitandao yake ya kijamii katika jaribio la kihistoria huko California, huku Ulaya sasa ikichunguza Snapchat kutokana na wasiwasi kama huo.

Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) zimekataa kumuunga mkono Rais wa zamani wa Senegal Macky Sall kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ili kuchukua nafasi ya Antonio Guterres. Kulingana na taarifa, jumla ya nchi 20 wanachama wa AU, ambazo hazikutajwa zimepinga ugombea wa Macky Sall, aliyeiongoza Senegal kuanzia 2012 hadi 2024 na ambaye pia hakuungwa mkono hata na nchi yake.

Nchini Kenya, uchunguzi wa miili huko Kericho unaendelea. Kaburi la watu wengi liligunduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika mji huu mdogo magharibi mwa nchi. Vijana, walioajiriwa kama wachimba makaburi na watu wasiojulikana, waliwaarifu polisi. Baada ya kufukua maiti, miili thelathini na mitatu iligunduliwa: watu wazima wanane na watoto ishirini na watano.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now