Watch FIFA World Cup 2026™ LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari: Onyo za mafuriko zawekwa kote jimboni Queensland

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Onyo za mafuriko zimewekwa kote jimboni Queensland, wakati hali ya hewa ya kitropiki inatabiriwa kufika pwani mchana wa leo kati ya miji ya Cairns na Townsville.


Mvua kubwa imesababisha mafuriko makubwa tayari katika maeneo ya Kaskazini usiku kucha, jeshi la polisi wakitoa onyo la dharura ya mafuriko kwa wakazi wa Daintree.

Australia inaendelea kujadiliana na mashirika ya ndege ya kibiashara katika Falme za Kiarabu [[U-A-E]], kwa ajili yakuwezesha safari zaidi za ndege kuwarejesha Waaustralia waliokwama Mashariki ya Kati. Ingawa maelfu ya raia wako katika eneo hilo, Idara ya Mambo ya Nje inasema si Waaustralia wote wanaotaka rudi nchini.

Bunge la Somalia limepiga kura ya kuifanyia mageuzi katiba yake na kuurefusha muhula wa wabunge na rais. Haya yamesemwa na spika wa bunge la nchi hiyo, hatua inayosogeza mbele kwa mwaka mmoja uchaguzi uliokuwa umeratibiwa kufanyika.

Mwanahabari kutoka nchini Burundi Sandra Muhoza, ambaye amekuwa akizuiwa tangu Aprili mwaka 2024 na baadaye kuhukumiwa jela miaka minne mwezi Januari, ameachiwa huru.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.


Share

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now