Taarifa ya Habari: Polisi wamkamata kakake Mfalme Charles

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Andrew Mountbatten-Windsor ameachiliwa huru chini ya uchunguzi baada ya polisi wa Uingereza kumhoji kwa saa muda wa masaa 12 kwa tuhuma za utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma.


Wanachama wa jumuiya ya Waislamu wa Sydney wanamsihi Seneta Pauline Hanson kutembelea Lakemba wakati wa Ramadhani na kuelewa vyema eneo hilo, baada ya kauli wanazosema zimechochea mgawanyiko. Hadi watu milioni moja wanatarajiwa katika soko maarufu la usiku la kitongoji hicho cha Sydney, ila mvutano umeongezeka tangu Seneta Hanson alipodai kuwa hakuna Waislamu wazuri.

Jumla ya Wakenya 1,000 wameajiriwa kupigania Urusi, kulingana na ripoti ya ujasusi ya Kenya inayoelezea mtandao wa maafisa wahalifu wanaodaiwa kushirikiana na makundi ya biashara haramu ya binadamu. Ripoti hiyo, iliyowasilishwa bungeni siku ya Jumatano na Idara ya Ujasusi ya Kenya (NIS), inasema Wakenya 89 walikuwa mstari wa mbele katika vita kati ya Urusi na Ukraine kufikia mwezi Februari mwaka huu.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.


Share

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now