Serikali ya Shirikisho imeagiza familia za wafanyakazi wa ubalozi wa Australia, na maafisa walioko Israeli na Lebanon kuondoka, ikitaja kuongezeka kwa mivutano katika eneo hilo. Tovuti ya Smartraveller imesasisha ushauri wayo wa usafiri, ikisema serikali imeagiza wategemezi wote wa maafisa wa Australia walioko katika nchi hizo mbili waondoke.
Waandishi wa habari 129 na wafanyakazi wa vyombo vya habari waliuawa duniani kote mwaka jana, hiyo ni idadi kubwa zaidi katika miongo mitatu ya utunzaji wa kumbukumbu za CPJ, huku theluthi mbili ya vifo vikihusishwa na moto wa Israel, kulingana na Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari.
Kundi la wanaume 17 wa Afrika Kusini ambao wanadaiwa kushawishiwa kupigania Urusi nchini Ukraine, wamerejea nyumbani kufuatia uingiliaji kati wa kidiplomasia. Imeripotiwa wanaume hao walidanganywa kwa ahadi za kazi za usalama, kabla ya kutumwa kupigana mashariki mwa Ukraine, jambo lililoibua wasiwasi kuhusu mitandao ya kuajiri watu inayowalenga raia wa Afrika kwa ajili ya vita.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.





