Mabadiliko ya kodi ya serikali ya shirikisho yamepitishwa ndani ya nyumba la Wawakilishi - ila, upinzani wa mseto hauja tupilia mbali uwezekano wa muungano na chama cha Greens kuzuia mabadiliko hayo kupitishwa ndani ya Seneti na kuwa sheria.
Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa
Mpango wa kuwaruhusu wanawake katika jimbo la New South Wales kupata dawa ya mpango wa uzazi, kupitia maduka ya dawa ya karibu unaanza kutumika leo. Kuna wafamasia 30 wanaostahiki ambao wamekidhi mahitaji ya mafunzo yaliyoidhinishwa ili kuweza kuandikia dawa hiyo, lakini idadi hiyo inatarajiwa kukua kwa kiasi kikubwa kadri wengine wanavyokamilisha mafunzo katika miezi ijayo.
Rais wa Kenya, William Ruto, amesema serikali yake inafanya jambo sahihi kwa kuruhusu Marekani kujenga kituo cha karantini ya Ebola nchini humo. Akizungumza akiwa katika ziara rasmi nchini Afrika Kusini, Ruto amesema itakuwa si jambo la kibinadamu kuikatalia Marekani ombi la kujenga kituo hicho kwa gharama zake.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.





