Licha ya ukosoaji huo Waziri Mkuu amepuuza ufichuzi katika ripoti ya tume ya muda ya kifalme kwamba, matumizi ya fedha katika kupambana na ugaidi 'yalipungua kwa kiasi kikubwa' kabla ya shambulio la kigaidi la Bondi. Ripoti hiyo imetoa mapendekezo 14 ikiwa ni pamoja na usalama zaidi katika matukio ya Kiyahudi, mapitio ya mifumo ya ujasusi ya Australia na sheria thabiti za kitaifa za bunduki. Licha ya kupendekeza mapitio ya mifumo iliyopo, jaji wa zamani wa Mahakama Kuu Virginia Bell, na mkuu wa tume amesema hakuna suala linalohitaji hatua za haraka lililotambuliwa.
Shirika la Anglicare Australia linasema uwezo wa kukodisha nyumba umepungua kwa kiwango cha chini kabisa. Picha yake ya hivi karibuni ya Uwezo wa Kukodisha Nyumba iliyofanyiwa utafiti ilifikia takriban orodha elfu 49 kote nchini, ikibaini kuwa kukodisha nyumba moja tu nchini kote kulikuwa nafuu kwa mtu anayetumia JobSeeker, na hakuna kwa mtu anayetumia Posho la vijana. Mtendaji mkuu wa shirika la Anglicare Australia Kasy Chambers, anasema swala la nyumba lazima lichukuliwe kama haki ya msingi.
Mwanamume mwenye uraia wa Uganda na Marekani, Christopher Okello Onyum, ambaye aliwaua kwa kuwachoma visu watoto wanne katika kituo cha kulelea watoto wachanga mapema mwezi huu, amehukumiwa adhabu ya kifo na mahakama jijini Kampala. Mauaji hayo ya kutisha yameibua wito wa kuimarishwa kwa usalama katika shule na vituo vya kulelea watoto ili kuzuia matukio kama hayo yasijirudie.





