Watch FIFA World Cup 2026™ LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari: Viongozi wa dunia wakubali kutoa idadi kubwa ya mapipa ya mafuta kutoka akiba ya dharura

Bench - Swahili.jpg

Mataifa tajiri zaidi duniani yamekubali kutoa idadi kubwa ya mapipa ya mafuta kutoka akiba ya dharura, kwa ajili ya kupunguza ongezeko kubwa la bei kutokana na vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.


Tahadhari ya dharura kuhusu mafuriko imetolewa asubuhi ya leo kwa wakazi wa Chinchilla magharibi mwa Queensland. Mafuriko yameathiri jamii kote jimboni Queensland, maji ya mafuriko hayo yakiwa mabaya zaidi kuikumba jamii ya kikanda katika zaidi ya muongo mmoja. Yame sababisha watu 200 kuhamishwa kutoka nyumba zao katika eneo la karibu la Bundaberg.

Mashambulizi ya anga yaliyotokea Goma yamesababisha vifo vya watu kadhaa katika mji huo muhimu wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Goma inadhibitiwa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda. Mashuhuda wamesema milio ya mabomu na sauti za ndege zisizo na rubani vilisikika katika mitaa kadhaa ya makazi ya Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini karibu na mpaka wa Rwanda. Watoa misaada ya kiutu wameripoti kuwa majengo kadhaa yalilengwa na watu kadhaa kupoteza maisha kufikia Jumatano asubuhi.

Watu 30 wamefariki dunia kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa katika eneo la Gamo kusini mwa Ethiopia. Mafuriko hayo yalitokea hasa katika maeneo ya Degama, huku mamlaka zikieleza masikitiko yao kutokana na vifo hivyo. Mvua kubwa imeendelea kushuhudiwa katika sehemu mbalimbali za Afrika Mashariki katika siku za karibuni. Nchini Kenya, makumi ya watu walipoteza maisha baada ya mvua kubwa kunyesha jijini Nairobi na maeneo mengine mwishoni mwa wiki.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa zaidi.


Share

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now