Jana Alhamisi Bunge la shirikisho lilipitisha sheria mpya kuongeza faini maradufu, kwa vituo vya mafuta vinavyo ongeza bei ya mafuta kwa njia bandia, hadi dola milioni 100.
Serikali ya shirikisho imesema wafanyakazi wanaolipwa mshahara mdogo zaidi nchini Australia, wanapaswa pewa nyongeza ya mishahara iliyo juu ya mfumuko wa bei mwaka huu na Tume ya Haki ya Kazi. Harakati ya vyama vya wafanyakazi inaomba ongezeko la asilimia 5 huku kundi la wafanyabiashara la Chama cha Biashara na Viwanda cha Australia likitaka ongezeko la asilimia 3.5.
Polisi jimboni Victoria wataongeza maradufu idadi ya maafisa katika eneo kuu la biashara la jiji la Melbourne. Uhalifu jimboni Victoria sasa uko katika kiwango cha juu zaidi katika kipindi cha miaka 10, na kuna uhaba wa polisi wakati nafasi zilizo wazi zikizidi maafisa 1300.
Wakazi wa mji mkuu wa Kenya, Nairobi, wana wasiwasi wakati bwawa lililoko kusini-magharibi mwa jiji liko katika hali ya hatari ya kuporomoka. Katika taarifa iliyotolewa wiki hii, Mamlaka ya Rasilimali za Maji ilionya kwamba miundombinu iko katika kiwango cha juu kutokana na mvua kubwa ambayo imenyesha katika mji mkuu katika wiki za hivi karibuni.Inawaomba wakazi wa vitongoji sita jijini humo kuhama. Kitongoji duni cha Kibera ni miongoni vitongoji hivyo.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.





