Watch FIFA World Cup 2026™ LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari: Vituo vya kuuza mafuta vyaonywa visiongeze bei kupita kiasi

Bench - Swahili.jpg

Mojtaba Khamenei ametangazwa kuwa kiongozi mkuu mpya wa Iran.


Bw Mojtaba ni mtoto wa marehemu, Ayatollah Ali Khamenei, ambaye aliuawa katika wimbi la awali la mashambulizi yaliyoanzishwa na Marekani na Israel wiki iliyopita.

Bei ya mafuta imezidi dola za Marekani 100 kwa pipa kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miaka mitatu na nusu, vita vya Iran vikizuia uzalishaji na usafirishaji kwa meli katika eneo la Mashariki ya Kati. Tume ya Ushindani na Watumiaji ya Australia imeonya vituo vya mafuta nchini Australia visitumie fursa ya mzozo wa Mashariki ya Kati kuongeza bei ya petroli kupita kiasi.

Watu 23 wamepoteza maisha jijini Nairobi nchini Kenya, kwa mujibu wa ripoti za polisi, kufuatia mvua kubwa iliyosababisha mafuriko usiku kucha kuamkia siku ya Jumamosi. Barabara nyingi za jiji la Nairobi, ziligeuka kuwa mito kwa sababu ya mafuriko, ambayo yamesababisha maafa na kuathiri makaazi ya maelfu ya watu, huku wenye magari wakisombwa na maji katika barabara kadhaa hasa ile ya kwenda Mombasa.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.


Share

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now