Watch FIFA World Cup 2026™ LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari:Wakazi wa Kusini Australia wa elekea debeni, je kutakuwa mabadiliko ya serikali?

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema usambazaji wa mafuta nchini Australia uko salama, lakini anataka Australia iwe tayari kupita kiasi linapokuja suala la kudhibiti uhaba wa mafuta nchini humu.


Ikiwa imesalia siku moja kabla ya uchaguzi wa jimbo, chama cha Labour cha Kusini Australia kina tarajiwa kusalia serikalini na kushinda uchaguzi huo kwa urahisi. Utafiti uliofanywa kwa niaba ya gazeti la The Australian, unaashiria chama cha Labor kikiwa na asilimia 40 ya kura za kwanza kuelekea uchaguzi wa kesho Jumamosi 21 Machi. Chama cha Liberal kinahitaji kushinda viti 11 vya ziada vya bunge la chini, ili kuchukua tena serikali na kumzuia kiongozi wa jimbo hilo Peter Malinauskas kushinda muhula wa pili. Ila chama cha upinzani cha Liberal kinapokea kura kwa asilimia 16 pekee wakati chama cha One Nation kikiwa na asilimia 22 ya kura hizo.

Waislamu kote duniani wanaadhimisha mwisho wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wakisherehekea Eid. Sikukuu ya Eid inajumuisha karamu ya kuvunja siku 30 za kufunga wakati wa Ramadhani. Asubuhi ya leo Ijumaa 20 Machi, Waziri Mkuu Anthony Albanese alijumuika katika sala, katika Msikiti wa Lakemba ambaa uko magharibi mwa Sydney.

Katika muktadha wa kukwamuwa mchakato wa amani mashariki mwa DRC ambao unaonekana kukwama, kufuatia kuendelea kushuhudiwa mapigano, Marekani iliwakaribisha wawakilishi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda mjini Washington siku ya Jumanne na Jumatano.

Polisi nchini Tanzania imetuhumiwa kutumia nguvu kupita kiasi kukandamiza waandamaji wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Ripoti ya Human Rights Watch (HRW), imeeleza hali ya kusikitisha iliyoikumba taifa hilo la Afrika Mashariki na kusababisha maafa ya mamia ya watu wakati na hata baada ya uchaguzi nchini humo.


Share

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now