Viongozi wa majimbo na wilaya wamemteua mratibu katika mkutano wa kitaifa wa baraza la mawaziri, kusimamia masuala yanayowezekana ya usambazaji na ongezeko la bei lililosababishwa na vita vinavyo endelea Mashariki ya Kati, wakati petroli na dizeli ya ziada ikitolewa kwa maeneo ya kikanda yanayokabiliwa na uhaba.
Takriban watu 500 wanatarajiwa kuhamishwa kutoka jumuiya ya Ghuba ya Carpentaria ya Numbulwar wakati Kimbunga chaki Tropiki cha Narelle kikijiandaa kuvuka pwani katika saa 24 zijazo. Shirika la huduma za dharura la SecureNT limesema watu hao wanatarajiwa kusafirishwa kwa ndege hadi Darwin katika siku zijazo.
Iran imetoa wito wa kuondoka mara moja katika vituo vya mafuta nchini Qatar, Saudi Arabia na U-A-E, kabla ya mashambulizi ambayo inasema yanaweza kutokea ndani ya saa chache zijazo. Makombora ya Iran tayari yameshambulia kitovu cha viwanda cha Ras Laffan cha Qatar katika hatua yakulipiza kisasi kwa shambulio kwenye uwanja wake wa gesi wa South Pars, wakati huo huo Saudi Arabia ikisema imezuia makombora yaliyolenga Riyadh na ndege isiyo na rubani inayolenga kituo cha gesi katika eneo la mashariki ya nchi hiyo.
Uingereza na Rwanda zitakutana katika Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi (PCA) huko The Hague kuanzia leo Jumatano, huku Kigali ikidai zaidi ya pauni milioni 100 kutoka kwa Uingereza. Maafisa kutoka nchi hizo mbili watawasilisha kesi yao katika kikao cha siku tatu mbele ya mahakama hiyo ya kimataifa iliyoanzishwa mwaka 1899 kusuluhisha mizozo ya kimkataba kati ya mataifa. Jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo ya PCA litasimamia kesi hiyo na huenda likachukuwa miezi kadhaa kutoa uamuzi.
Senegal imetoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu kile ilichodai kuwa ni ufisadi ndani ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) baada ya nchi hiyo kupokonywa taji la Kombe la Mataifa ya Afrika 2025.





