Tahadhari kwa wanaohitimu shule

schoolies.jpg

Kadri maelfu ya vijana wanaposherehekea kumaliza Mwaka wa 12, wanakumbushwa juu ya hatari zinazokuja na unywaji pombe, hasa nje ya nchi. Wazazi na marafiki wa waathiriwa wa sumu ya methanol, Bianca Jones na Holly Bowles, wamejiunga na juhudi mpya za usalama, wakiwatia moyo wasafiri vijana kuchukua maamuzi salama zaidi.


Kila mwaka, maelfu ya wahitimu wa shule nchini Australia husafiri nje ya nchi kwa mapumziko, kwa tukio linalojulikana kama "schoolies". Ni wakati ambapo vijana huanza safari zao za kimaisha - na wazazi hufanya dua. Kwa Michelle Jones, ambaye binti yake Bianca hakurudi kutoka likizo yake Laos, ni kumbukumbu yenye machungu na furaha.

Ni dhahiri sana, hasa kwenye lango la kuondoka pale ambapo tulisema kwa heri kwa wasichana wetu. ni dhahiri sana, inasikitisha sana
Michelle Jones

Bianca Jones na rafiki yake Holly Bowles walifariki baada ya kunywa vinywaji vilivyotiwa methanoli katika hosteli ya wasafiri mjini Vang Vieng, mwezi Novemba uliopita. Walikuwa na umri wa miaka 19

 Sasa, wazazi wao wanataka vijana wengine wajue hatari zinazokuja na kusafiri - na kunywa pombe - nje ya nchi. Mama wa Holly, Sam Bowles, anasema wanataka kuungana na wazazi wengine.

 
Inatugusa sana. Tunachojaribu kufanya ni kusambaza ujumbe ili kuwalinda wasafiri wengine
Sam Bowles
Familia ziko katikati ya kampeni mpya ya usalama inayowalenga wanafunzi wanaohitimu shule, iliyoanzishwa na serikali ya shirikisho katika ukumbi wa kuondoka wa kimataifa wa uwanja wa ndege wa Melbourne. [[Jumanne]]

 
Bianca na Holly walikuwa na furaha kuhusu kusafiri nje ya nchi pamoja. Wakati Bianca aliwasilisha wazo hili kwa Mark na mimi, tulikuwa na tahadhari kidogo, lakini pia tulijua kwamba kusafiri nje ya nchi na Holly ilikuwa jambo walilotaka kufanya na tulikuwa na uhakika kuhusu wao kusafiri pamoja. Walikuwa werevu na walijua jinsi ya kujitunza.
Sam Bowles
 Kampeni hii inawapa vijana na wazazi ushauri wa vitendo kuhusu kunywa kwa kiasi, kutunza marafiki, na hatari zinazoweza kutokana na vinywaji visivyolipishwa, vya bei nafuu au vinavyotia shaka.

 
Kuwa na tahadhari kuhusu matumizi ya pombe na vinywaji vyenye kama vile cocktails, buckets na shots
Sam

Kuna mwongozo wa jinsi ya kupata msaada mambo yakienda vibaya.
Inaungwa mkono na tovuti ya SmartTraveller na kikundi kisicho cha faida cha Drinkwise. Ujumbe utajumlisha matukio ya matangazo kwenye maeneo ya kuondokea katika viwanja vya ndege, na matangazo yanayolengwa kwa simu za rununu, kama anavyoeleza Mkurugenzi Mkuu wa DrinkWise, Simon Strahan.

Watakuwa wakiona hizo jumbe katika na kandokando ya viwanja vya ndege. Watakuwa wakiona hizo jumbe kwenye mitandao ya kijamii wanapotafuta baa. Itaonekana kama sehemu ya shughuli za utafutaji. Huko Australia, tutakuwa na jumbe hizo kwenye maduka ya pombe pia. Tunayo uhamasishaji, ambao utakuwa viwanjani, sehemu ya hiyo itakuwa ni kuhusika moja kwa moja na wahitimu wa shule, kuwapa bidhaa, vikumbusha vya sasa, na kweli kuanza kuzungumza nao
Sam Trahan

Kwa kufikia mwishoni mwa mwaka, kampeni inaongezeka kabla ya sherehe za wanaosherehekea kumaliza shule. Maelfu ya wanafunzi wanatarajiwa kusafiri ndani na nje, kwenda kwenye maeneo maarufu ya karamu kama Bali, Fiji, Gold Coast, na Asia.

 Waziri wa Elimu Jason Clare anasema kampeni hii ni kuhusu kuwafikia vijana popote walipo.

 
Tunataka muwe na furaha na tunataka muwe salama. Tunataka mrudi nyumbani salama, na hilo ndilo msingi wa kampeni hii - taarifa mtandaoni, kwenye ndege, katika uwanja wa ndege, ujumbe wa maandishi, mitandao ya kijamii, lakini pia kufikisha taarifa kwa shule.
Jason Clare

Licha ya uchunguzi mrefu na harakati za polisi huko Laos pamoja na shinikizo kutoka kwa mamlaka za Australia, bado hakuna mashtaka yaliyowekwa kuhusu vifo vya Bianca na Holly.

Michelle Jones na Sam Bowles wanakumbuka furaha ya binti zao wakati walipoanza safari yao ya kusisimua, lakini wanawasihi wazazi kuongea na watoto wao kuhusu kubaki makini.

 



"Wazazi wanapaswa kuwa na mazungumzo na kuwakalisha chini watoto wao, kabla ya kwenda zao.
Michelle Jones na sam Bowles

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service