Tangu kuanzishwa kwake 1999 na shirika la Yothu Yindi Foundation, Garma imekuwa jukwaa muhimu kwa mazungumzo kati yawa Australia wa Kwanza na jamii isiyo yawa Australia wa Asili.
Mbali na mada za kisiasa, mkazo pia ulikuwa kwa muziki, densi na kuchangia utamaduni.
Kila mwaka katika eneo la kaskazini mashariki Arnhem Land, tangu mwaka wa 1999, sherehe ya Garma huleta pamoja maelfu ya watu wanao jumuisha viongozi wa jamii ya Yolngu, familia, wamiliki wa utamaduni wa jadi, pamoja na wageni kutoka sehemu tofauti za Australia na dunia kwa siku nne za kujifunza utamaduni.