Siku ya 19 ya Kombe la Dunia la FIFA ilijumuisha mechi tatu za mchujo zenye ushindani mkali, huku Ujerumani na Uholanzi zikiondolewa baada ya mikwaju ya penati, wakati huo huo Brazil ilinyakua ushindi katika mechi yao muda mfupi kabla ya kipenga cha mwisho.
Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa
Mabingwa mara tano wa dunia Brazil wamefanikiwa kuingia katika Raundi ya 16, baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Japan, bao la ushindi likifungwa katika dakika ya mwisho ya ziada.
Jimboni Massachusetts, mabingwa mara nne wa dunia Ujerumani walipigwa kwa njia ya kushangaza na Paraguay, ambao walishinda 4-3 katika mikwaju ya kwanza ya penati ya mashindano hayo.
Mjini Monterrey, Mexico pambano lingine la kusisimua lilishuhudiwa kati ya Morocco ambayo katika nafasi ya sita na Uholanzi iliyo katika nafasi ya saba katika orodha ya timu bora duniani.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






