Wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza wanahimiza kila mtu apate chanjo ya mafua, kwa ajili ya kujaribu kuzuia kurudia kwa mwaka jana ambapo Australia ilishuhudia idadi kubwa ya vifo vilivyo sababishwa na mafua.
Zaidi ya watu 1,700 walifariki na kulikuwa na visa zaidi ya nusu milioni vilivyothibitishwa.
Wataalamu wa afya wanasema viwango vya chini vya chanjo vinachangia katika idadi kubwa ya visa hivyo. Wanaonya kuwa mwaka huu unaweza kuwa mbaya zaidi kutokana na kuenea kwa aina ya mafua yanayo julikana kama subclade K au Super-K.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.





