Wanafunzi 16 wamekufa katika mkasa wa moto, uliotokea katika mabweni ya shule moja ya wasichana katika Kaunti ya Nakuru nchini Kenya.
Hilo ni tukio la hivi karibuni la aina hiyo kulitikisa taifa hilo la Afrika Mashariki. Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba, amesema wanafunzi wengine 79 walijeruhiwa katika mkasa huo wa Shule ya Wasichana ya Utumishi, ambayo ina zaidi ya wanafunzi 800 katika eneo la Gilgil katikati mwa Kenya. Chanzo bado hakijabainika. Ogamba amesema mamlaka zitachunguza kama mwongozo wa usalama wa moto shuleni ulifuatwa.
Serikali ya Uganda imeamuru kufungwa kwa mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia ongezeko la visa vinavyoshukiwa kuwa vya aina mpya ya virusi vya Ebola.
Uamuzi huo umechukuliwa kufuatia taarifa kwamba wahudumu wa afya wa Uganda wameambukizwa virusi hivyo kutoka kwa wagonjwa waliotoka upande wa Kongo.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.






