Lisa Fox ni mama mwenye umri wa miaka arobaini na nne na anaishi katika Pwani ya Kati ya New South Wales.
Anakumbuka kupitia matatizo ya afya ya akili wakati wa kipindi cha prenatal alipokuwa mjamzito na alipozaa mtoto wake miaka 10 iliyopita. Wakati Lisa tayari alikuwa anaonwa na mtaalamu wa magonjwa ya akili na mwanasaikolojia, kwa ajili ya hali ya afya ya akili aliyokuwa nayo awali, anasema hakuwahi kupewa msaada maalum kwa kipindi cha prenatal.
Lisa anasema alihisi kujitenga na kutoshikamana wakati wa ujauzito wake na katika miezi kumi na mbili na kumi na nane baada ya kumzaa mtoto wake Luka.
Na kwa kweli, unajua, baada ya miezi 4 nilikaa karibu wiki 5 katika kituo cha afya ya akili kunisaidia. Na aibu inayokuja na hali hiyo, na jinsi aibu inavyopelekea kujitenga, ambayo ni hatari sana kwa jinsi mnavyoweza kujinasua kutoka katika hali hizi.Lisa Fox
Utafiti mpya uliofanywa na shirika lisilo la faida la afya ya akili katika kipindi cha ujauzito, Gidget Foundation, umebaini kuwa robo ya Waustralia wanaokumbwa na masuala ya afya ya akili katika kipindi cha ujauzito hawatafuti msaada.
Utafiti wa mwezi huu wa Novemba uliohusisha Waustralia zaidi ya elfu moja mia sita, ulibaini kuwa thuluthi moja ya watu walidhani dalili zao hazikuwa za kutosha kuwa na hofu. Mtaalamu wa saikolojia katika Gidget Foundation na meneja wa timu, Katie Peterson anasema hii inatokana na ukosefu wa kuelewa dalili na ishara za afya duni ya akili katika kipindi cha ujauzito.
Nafikiri inahusiana na watu kutokuelewa kabisa tofauti kati ya labda matatizo ya afya ya akili na changamoto tofauti zinazohusiana na kuzoea kuwa mzazi mpya. Kwa sababu kuna sababu nyingi katika kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua, ambacho tungechukulia kama vigezo vya hatari ya watu kuendelea kupata shida ya afya ya akili. Lakini ninavyofahamu ni kuwa kuingilia mapema ndiyo nzuri zaidi. Badala ya kusubiri mtu awe katika hali nzito au kali zaidi, tunataka kwa kweli watu washiriki na msaada wa kitaalamu mapema.Katie Peterson
Bi. Peterson anaelezea baadhi ya vigezo vya hatari kwa masuala ya afya ya akili yanayohusiana na kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua.
Watu wanapaswa kuzoea, haswa akina mama, wanapitia mabadiliko makubwa ya kihomoni, kimwili, kihisia, na hata katika majukumu yao ya kijamii. Kwa hivyo, kuna mambo mengi ambayo wazazi wapya wanapaswa kuelewa na kukabiliana nayo. Lakini pia tunaona kwamba wazazi wapya wanaweza kupitia uzoefu wa kiwewe cha kuzaliwa. Wanaweza kukumbana na hasara ya perinatal, wazazi wengine wanaweza kuwa na matatizo ya kiafya kwao wenyewe au kwa mtoto wao. Kwa hivyo ni wakati ambapo mambo yanaweza kwenda vibaya wakati mwingine. Na hii inaongeza mizigo ya ziada ya msongo wa mawazo.Katie Peterson
Aibu na unyanyapaa pia vina jukumu katika kuwazuia watu kutafuta msaada unaofaa. Afisa mkuu mtendaji wa shirika la afya ya akili ya perinatal PANDA, Julie Borninkhof, anaelezea.
Tunajua bado watu katika nchi hii, hasa kina mama zetu, wanaogopa kuanzisha mazungumzo kuhusu udhaifu kwa sababu wanatarajia mfumo na jamii itasema 'hamfai kuwa wazazi'. Na bado tunasikia kutoka kwa wapigaji simu kwamba wana wasiwasi watu watataka kuwanyang'anya watoto wao na kusema 'hamfai kuwa wazazi'. Na hiyo inazuia tabia ya kuomba msaada.Julie Borninkhof
Lisa anaamini kuwa na upatikanaji wa zana za afya ya akili za kujifungua zilizobinafsishwa ingemsaidia kukabiliana na hisia za aibu alizopitia wakati huo.
Kuwa na msaada maalum kwa wanawake katika kipindi cha perinatal ni muhimu sana kwa sababu hata nilipokuwa natafuta mwanasaikolojia binafsi na daktari wa akili, sikuweza kupata msaada kamili unaoweza kupokea unapokuwa mjamzito na kujifungua. Na vile vile, nilichojifunza zaidi ni kwamba mnawajibika kudai haki zenu wenyewe. Ni vigumu, lakini ni muhimu kudai mahitaji yenu. Mnaweza kusonga mbele na kutafuta wataalamu wengine wa kuwasaidia.Lisa Fox
Kuunganishwa na kuzungumza na akina mama wengine katika kipindi cha utoto wa mwanawe kulikuwa msaada mkubwa kwa Lisa jinsi alivyoelekeza afya yake ya akili.
nadhani jambo kuu kuhusu hali ya kutengwa inayojitokeza katika kipindi hiki ni kwamba mnaanza kuhisi kwamba hii ni mimi tu. Hii ni mimi tu, ni kosa langu, siwezi kumudu. Lakini mnapzungumza na wanawake wengine wanaopitia hali kama hiyo, mnaweza kusema, oh ndio, sawa, sio mimi tu, hii ni hali ya ulimwengu mzima inayoendelea. Hii ni kukosa usingizi. Hii ni ngumu sana.Lisa Fox
Bi Peterson anakubaliana kwamba kupunguza hali ya kutengwa na kuunda jamii za pamoja ni muhimu kuboresha upatikanaji wa huduma za afya ya akili kwa watu binafsi.
Wazazi wengi wanahitaji kusikia hadithi kutoka kwa mtu ambaye amepitia uzoefu wa moja kwa moja wa afya ya akili ya uzazi. Na kisha, wanaweza kuanza kuona jinsi wanavyohusiana na hadithi hiyo na kuona kwa nafsi zao. Na kwa kutambua kwamba hawako peke yao, inasaidia kupunguza aibu na unyanyapaa kuhusu kutafuta huduma za afya ya akili.Katie Peterson
Shinikizo la kifedha pia huchangia watu kuepuka msaada wa kitaalamu, na data kutoka The Gidget Foundation ikibainisha kuwa asilimia arobaini na saba ya wale waliohojiwa walitegemea sana miadi ya malipo madogo wakati wa kipindi cha ujauzito na asilimia ishirini na saba wakisema hawakuwa na uwezo wa kutafuta msaada.
Watu kutoka jamii za asili na za lugha tofautitofauti, pamoja na watu wa Mataifa ya kwanza, wanaweza pia kukutana na vizuizi vya kiasili na lugha, kama anavyoeleza Bi Peterson.
Tunajua kuwa kunaweza kuwa na ucheleweshaji wa kupata huduma zinazofaa kiutamaduni, waongoza lugha, na mara nyingine watu wenye asili za tamaduni tofauti au familia zilizo na utofauti wa kiutamaduni na lugha wanaweza kupata ugumu wa kuelewa au huduma hizo zinakuwa hazifai kiutamaduni. Pia, familia za Waaborijini na visiwa vya Torres Strait, kuna ongezeko la uwezekano wa changamoto za afya ya akili kipindi cha uzazi, na tena ni juu ya kupata msaada unaofaa kiutamaduni.Katie Peterson
Vilevile, mara nyingi kina baba huhisi kutengwa na huduma za afya ya akili kipindi cha uzazi - na ni zaidi ya asilimia tano tu ya watafutaji ushauri kwa simu wa PANDA ni wanaume, ingawa wanaume wanajumuisha asilimia kumi na nne ya watumiaji wa orodha ya ukaguzi wa afya ya akili. Hii ni kitu ambacho Bi. Borninkhof anaita the dad gap
Nadhani bado kuna aibu kubwa kwamba wanaume wanahisi wanapaswa kuwa nguzo katika familia, na mara nyingi tunazungumza kuhusu ukweli kwamba hata nguzo huvunjika. Na nadhani huduma bado ziko nyuma katika suala la kusaidia kina baba katika nchi hii. Kuna ongezeko kubwa na ukuaji katika msaada kwa baba, lakini bado zinajengwa kwa sababu uwekezaji kutoka kwa wafadhili na serikali haupo kwa kuwa tumekuwa tukijikita zaidi kwa akina mama.Julie Borninkhof
Lisa anasema jamii nzima inahitaji kuwa na ufahamu juu ya msaada wanaoweza kutoa kwa wazazi wapya.
Ninaamini ni jukumu la jamii. Ni familia, ni marafiki, ni maeneo ya kazi, kuelewa huduma za msaada zinazopatikana. Haitakiwi iwe ni mama pekee anayepambana ambaye kisha anahitaji kutambua kuwa anahitaji msaada - nyinyi nyote mnapaswa kufahamu hili.Lisa Fox













