Australia yafafanuliwa:waathiriwa wa ukatili wa kijinsia wahimizwa kuripoti

Chrissy struggled to navigate the legal system (Supplied).jpg

Nhân vật Chrissy trong bài

Mmoja kati ya wanawake watano na mmoja kati ya wanaume kumi na sita wamekumbwa na ukatili wa kingono wakiwa watu wazima huko Australia, kulingana na Ofisi ya Takwimu ya Australia ya 2023 - na bado asilimia tisini na mbili ya wanawake hawaripoti unyanyasaji wao wa hivi karibuni wa kingono. Ripoti mpya inataka kuelewa kwa kisheria miongoni mwa waathirika, huduma za mstari wa mbele, na wataalamu wa sheria, ili kusaidia waathirika kuifahamu mifumo changamano ya haki za jinai na kushughulikia viwango vya juu vya kuacha kesi za unyanyasaji wa kingono.


Na kwa kweli sikuwa na kidokezo chochote kuhusu nilichokuwa nikifanya. Nakumbuka tu kuwa na hofu sana kwa sababu nilihisi sina uwezo.
Chrissy
 

Hayo ni maelezo ya Chrissy, mwenye umri wa miaka thelathini na tatu, akirejelea uzoefu wake mgumu wa kuvuka mfumo wa haki ya jinai kama mwathiriwa na mnusurika wa unyanyasaji wa majumbani na kingono. Chrissy ni miongoni mwa waathirika-mnusuriko wengi wanaohisi kukosa nguvu kutokana na ukosefu wa maarifa kuhusu taratibu na mifumo ya kisheria katika kesi za unyanyasaji wa kingono.

 

Mama huyu anayeishi Wollongong alilazimika kwa mara ya kwanza kuvuka mfumo wa haki ya jinai mwaka 2021, wiki chache tu baada ya kujifungua. Chrissy alipata ujauzito wiki mbili baada ya kukutana na mnyanyasaji wake mwezi Mei 2021, na anasema alipitia karibu aina zote za unyanyasaji kutoka kwa mnyanyasaji wake karibu tangu mwanzo wa uhusiano wao - ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kihisia, kimwili na wa kingono.



Chrissy alikutana kwa mara ya kwanza na polisi baada ya mnyanyasaji wake kutoa taarifa ya uongo kwamba alikuwa amepotea pamoja na mtoto wake. Kilichofuata ni safari ndefu na ya kihisia ya miaka mitatu na nusu ya kisheria ambayo hatimaye ilisababisha mnyanyasaji wake kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela mapema mwezi huu kwa makosa matano kati ya manane yaliyowasilishwa dhidi yake.

Na nakumbuka nilipokuwa nimeketi hapo nikifikiria, nifanye nini? Sina wazo lolote la ninachogongana nacho. Na kwa kweli sikuwa na fununu nilichokuwa nikijikuta ndani. Ninakumbuka tu nikiogopa sana kwa sababu nilihisi sina uwezo tena. Uwezo wangu ulikuwa mikononi mwa mtu mwingine. Hadithi yangu ilikuwa mikononi mwa mtu mwingine. Msongo wangu, matokeo ya msongo wangu, yalikuwa mikononi mwa mtu mwingine.
Chrissy
 

Hadithi kama za Chrissy ndizo zinazo chochea ripoti mpya ya shirika la utetezi wa unyanyasaji wa kijinsia 'With You We Can'.

 Inasema jinsi pengo la uelewaji wa sheria linavyo wakosesha waathirika wa unyanyasaji wa kingono, na inapendekeza njia za kuboresha mfumo.

Sarah Rosenberg ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo na anasema hofu ni sehemu moja tu ya kutojali kwa waathirika katika kushughulikia mfumo.

Lakini pia waathiriwa hawajui jinsi ya kuanza kuelekea mahali pa kupiga ripoti. Ni vigumu sana kutoa taarifa, hakuna anayewafundisha namna ya kufanya hivyo. Ilinichukua vituo vitatu tofauti vya polisi kufikia hatua ya kusaini taarifa rasmi ya polisi. Na hivyo, mfumo huu ni wa ajabu. Mfumo wenye vikwazo vingi kupita kiasi ili tu mtu aweze kuingia, ni mfumo unaowazuia watu ambao wanahitaji zaidi upatikanaji wake.
Sarah Rosenberg
 

Chrissy alikabiliwa na vikwazo kila hatua alipopita. Ingawa anakumbuka mawasiliano mazuri ya mwanzo na afisa wa polisi, afisa upelelezi tofauti alimwambia alikuwa anapoteza muda alipoenda kituoni kutoa taarifa.

Ripoti ya With You We Can inasema viwango vya kupotea ni vya juu katika hatua ya polisi ndani ya mfumo wa haki ya jinai kwa kesi za unyanyasaji wa kijinsia. Ripoti inasema hili kwa kiasi kikubwa , linatokana na polisi kuongozwa na hitaji la ushahidi ili kuthibitisha hatia, badala ya kushughulikia uhalifu wenyewe, na bado wanaegemea sana kwenye nadharia potofu kuhusu ubakaji.
Bi Rosenberg anasema inahitajika zaidi ya mafunzo yanayozingatia athari za kiwewe ili kutatua mapungufu haya.

 
Na kwa hivyo, nadhani inapokuja kwa polisi, mbali na, bila shaka, hitaji la mafunzo kila wakati, na haswa mafunzo ya ufahamu wa kisheria vilevile, wanahitaji jukumu la lazima la kuchunguza. Kazi moja ambayo watu wengi, umma wa jumla wanafikiria kuwa polisi wanayo ni kuchunguza uhalifu, lakini kwa kweli hawana wajibu wa kutekelezeka wa kuchunguza uhalifu wa kijinsia. Na wakati hilo halijaamriwa, nia nzuri inaweza kutoka katika mafunzo, lakini bado mnaweza kuwa na afisa atakayempuuza mtu kwenye mlango.
Sarah Rosenberg

Waathirika manusura wanaofaulu kupita hatua hii ya awali na kuendelea hadi kesi mahakamani hukabili vikwazo vipya. Chrissy anakumbuka kumuona kwa kifupi mtuhumiwa wake kwenye skrini, licha ya kuhakikishiwa kwamba hatalazimika kumwona ikiwa atatoa Ushahidi.

 Chrissy, Mwenye umri wa miaka thelathini na tatu anaugua tatizo la neva ambalo linamaanisha mwili wake hushindwa kufanya kazi ipasavyo anapokabiliwa na viwango vya juu vya msongo. Katika siku ya nne ya kutoa ushahidi, Chrissy anasema alipata mshtuko na alichukuliwa hospitalini.

 Aliporudi siku iliyofuata, Chrissy anasema ulinzi ulitumia uzoefu wake dhidi yake kwa njia tofauti, ikiwa ni pamoja na kumshutumu kwa kutumia muda hospitalini kupitia ushahidi wote na kubadilisha majibu yake, licha ya kutokuwa na ufikiaji wa ushahidi nje ya chumba salama ambapo alionekana mahakamani.

 
Nilinifanya nihisi kuwa kwa sababu nilikuwa na mshtuko, nilikuwa nimekosea. Na hiyo ndiyo kitu kizima. Mnahisi kama nyinyi ndio mko kwenye jaribio. Kila mnalosema linahukumiwa. Kila mnalofanya linahukumiwa. Na kisha nina shida ya utengano. Kwa hiyo wakati huo, mojawapo ya siku za mwisho kabisa, yeye alijaribu kusema kwamba kwa sababu ya shida yangu ya utengano, nilikuwa na utu tofauti ambao ulikuwa na uhusiano na mnyanyasaji wangu.
Sarah Rosenberg
 

Bi. Rosenberg anasema hata wataalamu wa sheria katika mfumo mara nyingi hawajaandaliwa kutoa haki ya kisheria kwa utaratibu unaofaa.

 
Hata watu ambao wanapaswa kufanya kazi hiyo hawajafahamu maelezo ya kina yanayotokea katika kesi za udhalilishaji wa kijinsia au yale ambayo hayafanyiki katika kesi hizo, ambayo ni kudumisha ulinzi wa kisheria ili waathirika wapate haki kisheria. Zaidi ya hukumu ya hatia ambayo mngeita kama matokeo ya haki ya msingi, hukumu ya hatia au kutokuwa na hatia, haki ya kisheria ni kuhusu kama mambo yaliyotarajiwa kutokea yalifanyika, kama mlitendewa kwa heshima na staha.
Sarah Rosenberg
 

Waathirika hawapokei ushauri wa kisheria kutoka kwa waendesha mashitaka kwani wao ni mashahidi kwa kesi ya serikali dhidi ya utetezi.

Chrissy alilazimishwa kusafiri katika maeneo tofauti kwa sababu ya mashitaka yake ya unyanyasaji wa nyumbani na kijinsia na anasema kwamba angeona kuwa na uwakilishi huru wa kisheria ni msaada mkubwa.

Nadhani kile ambacho watu wengi hawatambui ni kuwa waathirika ni mashahidi. Nyinyi ni mashahidi tu. Hamna kile ambacho utetezi unacho. Hamna timu ya kisheria inayofanya kazi moja kwa moja nanyi. Nakumbuka wakati mwingine maswali yaliulizwa kwangu, na natamani kungekuwa na mtu ambaye angeweza kuniongoza, kunitayarisha.
Chrissy

Moja ya mapendekezo makuu ya ripoti hiyo ni kujumuisha ofa ya uwakilishi wa kisheria huru kwa waathirika na kufadhili mahakamani.

 Bi Rosenberg anasema hili ni muhimu hasa kwa makundi yenye mazingira magumu ambao wamepitia ubaguzi kutoka kwa polisi na wana uhusiano uliojengwa kwa kutokuwepo kwa imani - ikiwa ni pamoja na watu wa mataifa ya kwanza na watu wa LGBTIQ+, pamoja na watu wenye ulemavu, wafanyakazi wa ngono, au wale ambao wana visa vya muda.

 
Si kuhusu kusema tuwaweke wahanga kama chama katika mfumo wetu wa vyama viwili, na hivyo ingeweza kubadilisha mambo kwa kiasi kikubwa. Haki ya mtuhumiwa kupata kesi ya haki haitavunjwa. Kwa hakika, inainua na kudumisha mfumo mzima kufanya kazi kwa uadilifu. Ni kuhusu kuwaunga mkono waathiriwa ambao ni mashahidi wakuu katika kesi ya serikali dhidi ya mtuhumiwa, ili watoe ushahidi wao bora zaidi, bila kudhalilishwa, kusumbuliwa na kubatilishwa kwa njia isiyo halali.
Sarah Rosenberg
 

Australia tayari inaendesha majaribio ya uwakilishi huru wa kisheria katika baadhi ya majimbo, ikiwa ni pamoja na A-C-T, Victoria na Australia Magharibi.

Ripoti ya " With You We Can inasema uwakilishi huru wa kisheria ungebadilisha miili iliyogawanyika ya watetezi na kuwa moja yenye sifa ya kisheria katika mchakato mzima, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa kesi katika polisi, mahakama na hatua baada ya kesi, pamoja na ufafanuzi wa kisheria wa michakato, haki na maamuzi ili kuunga mkono bora uchaguzi wa waathiriwa

 

Mwakilishi hatabadilisha mashtaka na atahusika tu katika hali maalum, kama vile wakati masuala ya usiri yanapotokea katika kesi ambapo kunaweza kuwa na hati ya kuitwa mahakamani kwa rekodi za matibabu au ushauri. Daktari Rachel Killean ni Mhadhiri Mwandamizi katika Shule ya Sheria ya Sydney na anasema ingawa anaamini kuna nafasi ya uwakilishi huru wa kisheria katika kesi za unyanyasaji wa kingono, hatua zinahitajika ili kuhakikisha mtuhumiwa ana upatikanaji wa kesi ya haki.

 Uelewaji wa mapema wa kisheria kuhusu kesi za shambulio la kijinsia ni pendekezo jingine lililotolewa na ripoti, ikitaka masomo hayo kujumuishwa katika programu za ridhaa shule na vyuo vikuu.

Daktari Killean anakubaliana kuwa uelewa wa kisheria ni muhimu, lakini anaamini kuwa mabadiliko halisi kwenye mfumo yatatokea kwa kujumuisha mbinu zinazozingatia athari za kiakili katika kila hatua ya mchakato wa haki za jinai.

Chrissy anasema anazungumza kuhusu uzoefu wake kwa matumaini kwamba wengine watahisi kuwa hawako peke yao wakati wanapotafuta haki.

 
Kama nyinyi au mtu mnayemfahamu mnataka kuzungumza kuhusu unyanyasaji wa kingono au udhalilishaji, vurugu za kifamilia au za nyumbani, piga simu kwa 1800RESPECT kwa mojananesufurisufurisabatatusaba au tembeleeni www.1800RESPECT.org.au. Katika dharura, pigeni 000.

 


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service