Hamza alikuja Australia kutoka Saudi Arabia mwishoni mwa 2022 na karibu amemaliza digrii yake. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 amepoteza idadi ya udanganyifu aliyotakiwa kukwepa – ikiwa na simu ya kutia shaka miezi michache tu iliyopita.
Walikuwa wakiongea kuhusu punguzo kwa zawadi ya magodoro ya kitanda. Na nikawaambia, jina la kampuni ni gani? Hawataki kunipa jina la kampuni. Wao walikuwa tu kama, tuma maelezo ya akaunti yenu ya benki, kisha tutapeleka godoro kwenu. Nilikuwa na hisia kwamba ni ulaghaiHamza
AFP inasema inaona wanafunzi wa kimataifa zaidi wakiombwa kuuza maelezo yao ya benki na kitambulisho. Mkuu wa Uchunguzi Marie Andersson ametoa onyo la dharura kwa wanafunzi wanaoondoka Australia baada ya chuo kikuu.
Wanatoa pesa taslimu haraka... kisha mali hii hutumiwa kufua mapato ya uhalifu, mashambulizi ya uhalifu mtandaoni. Pia wanawadanganya waathiriwa watumie utambulisho bandia.Marie Anderson
Msimamizi anasema wanafunzi wanaweza kufikiwa na vyama vya kihalifu vinavyoonekana kuwa vya kisheria ambavyo vinatoa mamia ya dola kwa matumizi ya akaunti yao ya benki ya Australia.
Nyaraka za utambulisho kama passporti, leseni za kuendesha gari au kitambulisho kilichotolewa na serikali pia vinaweza kutumiwa kufungua akaunti za benki kwa jina la waathiriwa.
AFP inasema inachunguza mitandao zaidi ya ulaghai inayorejea kwenye akaunti za wanafunzi na inawafungulia mashtaka wale wanaohusika.
Wanaweza kuwa wanakabiliwa na mashtaka ya jinai kwa utakatishaji fedha au udanganyifu... Hii inaweza kuwa matokeo ya kukataliwa au kufutwa kwa visa, marufuku ya kudumu ya kuingia au kuingia tena Australia.Marie Anderson
Onyo hili linatolewa mwishoni mwa mwaka ambapo wanafunzi wanamaliza digrii zao na kufanya uamuzi kuhusu kubaki Australia au kurudi nyumbani. Mkuu wa Polisi anasema hii inaweza kuwa wakati wa hatari kwa ulaghai.
"
Kwa kuwa inaonekana wanarejea nyumbani katika siku chache zijazo, ni fursa nzuri sana ambayo haiwezi kukataliwa. Na wahalifu wanajua hilo. Ndiyo sababu wanawalenga wale wanafunzi... Tunataka kuhakikisha kuwa wanafunzi wa kimataifa wametolewa katika hiyo fomula.Marie
Mishween alikuwa mwanafunzi wa zamani kutoka india. Anasema aliibiwa dola elfu kumi kwa ulaghai wa bandia wa ATO mwaka elfu mbili ishirini namoja.
Ni kitendo kisichokuwa cha kibinadamu. Kulikuwa na milango mingi iliyofungwa mara baada ya mimi kusema kwamba mimi ni mwanafunzi wa kimataifa. Njia pekee ya kutoka katika hali hii ni kuwa na ufahamu wa haki zenu.Mishween
Wanafunzi wamepewa ushauri wasitoe maelezo yao ya kibinafsi kwa yeyote wasiyemfahamu, waseme hapana kama mtu anaomba kutumia au "kukopa" akaunti yao ya benki, na wakatae ofa zozote zenye mashaka.
Kwa yeyote ambaye ni mwathirika wa ulaghai - AFP inawashauri kusitisha mawasiliano na mlaghai na kuripoti. Kwa wakati huu, Hamza bado ana semester nyingine ya masomo na hajui kama atabaki Australia. Lakini anasema atabaki makini.
Inakera. Kama naondoka au nafika tu hapa, bado inakera mwishoni mwa siku... Kwa hivyo ni lazima tu kuendelea kuwa na umakini. Na hayo tu ndio ninayoweza kusemaHamza





