Waziri wa uhamiaji wa Australia ame thibitisha kuwa mtoto anaye julikana kama Asha kutoka familia ya waomba hifadhi, hata rejeshwa katika kizuizi kisiwani Nauru kwa sasa, ila siku moja ata rejeshwa huko. Asha pamoja na familia yake wame pewa hifadhi ndani ya jumuiya chini ya ulinzi wa idara ya uhamiaji. Hatua hiyo ilifikiwa baada ya madaktari hapo awali kukataa kutoa idhini ya Asha kuondolewa hospitalini hadi makazi yanayo stahili yatakapo patikana.
Share





