Serikali ya Turnbull ime hamasishwa iunde fursa zingine za kuwapa uhamisho wakimbizi wa ziada nchini Australia, kupitia mradi wa udhamini wa jamii.
Licha ya ripoti za mjadala ndani serikali ya mseto kuhusu mbinu zakupunguza idadiya wahamiaji ambao Australia inapokea, wanaharakati wa haki za wakimbizi wame ihamasisha serikali iunde nafasi za ziada elfu tano katika mradi wakibinadam kila mwaka, nakuiongeza hadi nafasi elfu kumi katika miaka mitano ijayo.
Share






