Mratibu Ulimbwende wa Ulimwengu maarufu kama 'Miss Universe kwa upande wa Tanzania Maria Sarungi, ameonyesha wasiwasi wake juu ya mashindano hayo baada ya makosa makubwa kufanywa kihistoria ya kutangazwa matokeo katika siku ya fainali hizo za urembo za kila mwaka za Kimataifa nchini Marekani.
Akiongea na Frank Mtao wa SBS Swahili kwa njia ya simu kutoka Tanzania baada ya kuwasili kutoka Marekani, Maria alieleza kosa lililofanywa na Steve Harvey katika kumtangaza mshindi, litalitikisa shindano la urembo hilo ikiwa mipango endelevu haitowekwa kuzuia maafa zaidi.
Share





