Sekta ya mavazi ya mazoezi inathamani yamabilioni ya dola, na kwa muda mrefu makampuni makubwa yakimataifa yame tawala sekta hiyo.
Cynthia ni mjasiriamali mchanga ambaye anaingia katika sekta ya kuuza mavazi yakufanyia mazoezi, ambako mavazi yake niyakipekee kwa sababu yanawapa wanawake wenye miili ya kila aina, fursa yakufanya mazoezi kwa starehe baada yakutokuwa na fursa yakupata mavazi hayo kwa muda mrefu.
Ali eleza idhaa ya Kiswahili ya SBS kuhusu mavazi yake yakufanyia mazoezi kwa jina la; Fit With Curves Active Wear na jinsi atakavyo kabiliana na makampuni makubwa yakimataifa, katika soko hilo la mavazi yamazoezi. Kwa taarifa ya ziada kuhusu mavazi ya mazoezi ya Cynthia tembelea tovuti yake: www.fitwithcurvesactivewear.com.au
Share





