Uvumi ulikuwa ume sambaa kwa miezi kadhaa na hofu ilikuwa imeongezeka kuwa, uchaguzi wa urais ambao ulikuwa ume pangwa nchini DR Congo, hauta fanywa kama ilivyo kuwa ime ratibiwa mwezi Novemba 2016.
Uvumi huo ulithibitishwa baada ya mkutano ulio jumuisha viongozi wakiraia, dini, siasa na Rais Joseph Kabila.
Mkutano huo ulikamilika kwa maafikiano yaku ipa tume ya uchaguzi ya taifa hilo, hadi mwezi Aprili 2018 kuandaa uchaguzi wa urais.
SBS Swahili ilizungumza na baadhi ya viongozi wa vikundi wa vijana walio changia maoni yao kuhusu uamuzi waku ahirisha uchaguzi wa urais nchini DR Congo
Share





