Kama simu yako kwa 000 siyo ya dharura, unaweza kuwa unawachelewesha watu ambao wako katika hali zinazo tishia maisha kupewa huduma kwa wakati.
Nchini Australia (000) ni namba ya huduma ya dharura ambayo unaweza tumia kuitisha gari ya dharura yawangonjwa, huduma yawazima moto au polisi unapo kuwa katika hali yakutishia maisha, au katika dharura ambayo ni mhimu sana kupokea huduma kwa wakati.
Kulingana na mamlaka ya huduma za dharura kwa simu (ESTA), katika miaka ya 2019-2022 kulikuwa idadi ya takriban simu elfu 7,600 zilizo pigwa kila siku kwa 000 jimboni Victoria pekee, au simu moja kila sekunde 11. Kwa taarifa zaidi kuhusu makala haya tembelea tovuti hii: www.triplezero.gov.au