Ongezeko hilo la visa vya COVID-19 jimboni Victoria, limesababisha majimbo hayo mawili kufunga mpaka unao ziunganisha, kwa ajili yakudhibiti usambaaji wa maambukizi.
Bi Marian kutoka kitengo cha huduma yawakimbizi katika idara ya afya ya NSW, ame eleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS jinsi shirika lake linavyo wa andaa watu walio wasili nchini hivi karibuni kama wakimbizi, kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na jinsi yakuepuka maambukizi ya virusi hivyo.