Wizara ya afya Tanzania imesema kuwa maambukizi ya wagonjwa wa mafua makali ya Influenza na Uviko-19 yameongezeka na kuwataka wananchi kuchukua hatua stahiki za kujikinga na maambukizi hayo.
Taarifa hiyo iliyotolewa na mganga mkuu wa serikali Dk. Grace Magembe imetokana na kufuatilia mwenendo wa magonjwa ya mlipuko.
Wizara hiyo imeongezea kuwa mafua makali ya Influenza na Uviko-19 huenezwa kwa kugusa mazingira yaliyochafuliwa na majimaji yanayotoka kwa mgonjwa na kuongeza kuwa dalili zake ni homa kali, kikohozi, mafua, maumivu ya kichwa na mwili.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.
Share






