SKIP TO MAIN CONTENT

Australia Yafafanuliwa:Je, unaweza chuma matunda kutoka bustani ya mtu?

Verge planting.jpg
A verge garden in Freemantle, WA. Credit: City of Fremantle

Ukitembea katika kitongoji cha Australia, unaweza ona kila kitu kuanzia majani ya kari na limau hadi nyanya na mimea inayokua katika bustani za mbele au kwenye ukingo. Lakini je, ni halali kuvivuna? Mwongozo huu unaelezea wakati ni halali kuvuna mazao, kwa nini ruhusa ni muhimu, na jinsi bustani za jamii zinavyotoa njia nyingine ya kukuza chakula chako mwenyewe.


Published

By Phil Tucak

Presented by Gode Migerano

Source: SBS



Skip to podcast episode content

Ukitembea katika kitongoji cha Australia, unaweza ona kila kitu kuanzia majani ya kari na limau hadi nyanya na mimea inayokua katika bustani za mbele au kwenye ukingo. Lakini je, ni halali kuvivuna? Mwongozo huu unaelezea wakati ni halali kuvuna mazao, kwa nini ruhusa ni muhimu, na jinsi bustani za jamii zinavyotoa njia nyingine ya kukuza chakula chako mwenyewe.


Key Points

  • Taking produce from someone else's garden without permission can be considered trespass and theft.
  • Always ask the resident's permission before taking produce from a garden or verge, unless it has clearly been left out for people to take.
  • Join a community garden in your local area to grow and share produce.

Je, naweza chukua mazao kutoka bustani ya mtu mwingine au ukingoni?

Ukiona matunda yaliyoiva kwenye bustani ya mtu, inaweza kuwa jambo la ushawishi kuyachuma.

Lakini kama Jarrad Duggan, anayeongoza timu ya usalama wa jamii katika Jiji la Fremantle, anavyoelezea, kuchukua mazao kutoka kwenye bustani ya mtu mwingine ni kinyume cha sheria.

"Kwa kweli si halali kuingia kwenye mali ya mtu yeyote bila ruhusa yake. Kwa hivyo hapana, hutaweza kutembea tu kwenye ardhi ya mtu na kuchukua chochote kutoka kwenye mali yake kwa sababu hiyo inaweza kuchukuliwa kuwa wizi," Bw. Duggan anasema.

Kwa maneno mengine, muulize mmiliki wa mali kila wakati kabla ya kuchukua mazao. Kanuni hiyo hiyo kwa ujumla inatumika kwa mazao yanayokua ukingoni nje ya nyumba ya mtu.

"Kwa upande wa ukingo, tena, si halali kuchukua chochote kutoka kwa yeyote kati yao. Ninajua ni ardhi ya baraza, lakini kwa kweli unahitaji ruhusa ya kuondoa chochote kutoka ukingoni," Bw. Duggan anasema.

"Unahitaji ruhusa kutoka kwa mtu anayeishi katika mali hiyo au anayemiliki mali hiyo. Ruhusa hii haitoki kwa baraza. Kwa kweli ni kutoka kwa mtu huyo."

Verge tree.jpg
Huenda ikawa jambo la kushawishi kuchuma matunda kutoka kwenye mti wa jirani—lakini je, ni halali? Credit: Pexels/Strannik-sk

Ni adabu gani nzuri kama naona mazao katika bustani ya mtu?

Ukitaka kuchukua mazao kutoka bustani au ukingoni mwa mali ya mtu, hatua ya kwanza ni rahisi: uliza.

"Kwa hivyo utahitaji ruhusa kila wakati—unaweza kufanya hivi kwa kugonga mlango, au unaweza kuwaachia barua ya heshima. Na ukipata ruhusa, ni vizuri kuwauliza ni kiasi gani unaruhusiwa kuchukua, na usiharibu mmea," Bw. Duggan anasema.

Watu wengi wanafurahi kuchangia mazao yao ya ziada, haswa ikiwa umeomba kwanza. Baadhi hata huacha matunda au mboga nje na bango linalowaalika wengine kuyachukua.

"Mfano unaokuja akilini ni kwamba unaweza kutembea barabarani na unaweza kuona sanduku dogo la kadibodi lililo karibu na bango linalosema 'bure' na linaweza kuwa limejaa limau, na hiyo ni ishara wazi kwamba wanatoa hii bure. Kwa hivyo katika hali hiyo, hutahitaji ruhusa," Bw. Duggan anasema.

Andrea Sciubba.jpg
Andrea Sciubba aacha nje limao za ziada kwa matumizi ya majirani wake. Credit: Josh Jenkins

Hilo ndilo hasa ambalo mkaazi Andrea Sciubba hufanya mara kwa mara katika kitongoji chake cha Nedlands huko Perth.

“Nina mti wa limau wa zamani sana kwenye bustani ya nyuma ya nyumba na nina bahati sana kwamba kila mwaka huwa inazaa matunda mengi.”

Ninachagua kadri niwezavyo, na ninaziweka kwenye sanduku na kuziacha karibu na sanduku la barua ili watu waweze kujisaidia.
Andrea Sciubba

Je, naweza panda mazao nje ya nyumba yangu?

Kingo, au ukanda wa majani, nje ya nyumba kwa ujumla ni ardhi ya umma inayosimamiwa na baraza la mtaa. Hata hivyo, mmiliki au mkaazi wa nyumba iliyo karibu kwa kawaida huwajibika kwa matengenezo ya kawaida, kama vile kukata nyasi.

Ikiwa unaruhusiwa kupanda matunda, mboga mboga au mimea kwenye ukingo wako inategemea sheria za baraza lako la mtaa.

"Kwa hivyo hii inatofautiana kutoka baraza hadi baraza. Baadhi wanaweza kuruhusu, wengine wanaweza kuizuia kabisa," Bw. Duggan anasema.

Bustani ya jamii ni nini?

Kama huna nafasi ya kulima chakula nyumbani, kujiunga na bustani ya jamii kunaweza kuwa chaguo lingine.

Bustani ya Jumuiya ya Hurstville katika kitongoji cha Sydney ina eneo la bustani la pamoja na viwanja zaidi ya 30 kwa wakulima wa bustani binafsi, kama mwanachama Sofia Carvajal anavyoelezea.

"Ni njia bora ya kujifunza, hasa kama wewe ni mgeni, kutoka kwa watu ambao wamekuwa wakifanya hivyo kwa miaka mingi. Unajifunza mengi kuhusu jinsi ya kupanda matunda na mboga... Pia unajifunza jinsi ya kufanya kazi pamoja kama kikundi, jambo ambalo ni muhimu sana."

Urban produce.jpg
Mazao yanaweza kuonekana mara nyingi yakikua kwenye bustani ya mbele. Credit: Pexels/Ivy Nguyen

Washiriki katika bustani ya jamii hujifunza kuhusu udongo na mbolea, mimea ya kupanda, na jinsi ya kuitunza.

"Kila bustani ya jamii hufanya kazi tofauti, lakini nadhani jambo kuu ambalo zote zinafanana ni kwamba una kipindi cha kujifunza kwanza na kisha unaweza kupanda kitu, na utaweza kuchukua kitu nyumbani mwishowe," Bi. Carvajal anasema.

Faida ya bustani ya jamii ni gani?

Bustani za jamii ziko wazi kwa watu wa asili zote, ingawa uanachama na orodha za kusubiri hutofautiana. Nyingi hutoa vifaa utakavyohitaji ili kuanza.

Bustani za jamii ni njia nzuri ya kukuza chochote ulicho nacho katika nchi yako ambacho huwezi kukipata kutoka duka lolote.
Sofia Carvajal

Mbali na fursa ya kulima mazao, bustani nyingi za jamii pia huendesha shughuli kwa watu wa rika zote.

"Kama una watoto, unaweza kuwa sehemu ya kusoma vitabu bustanini...Tuna programu nyingi sana kwa watu wa rika zote. Pia tuna programu kwa jamii zenye viwango tofauti vya uelewa kuja na kuwa na shamba. Ni jambo la kutuliza sana. Tumekuwa na programu kuhusu kutopoteza taka, kutengeneza mbolea, [na] kilimo cha kudumu. Huu ndio umuhimu wa bustani za jamii—inajumuisha sana katika suala la kuunda jamii," Bi. Carvaja anasema.

Kwa hivyo, iwe unataka kuchangia mazao mapya au kukuza yako mwenyewe, bustani za jamii hutoa njia ya vitendo ya kuchangia. Na ukiona matunda au mboga zikikua kwenye bustani ya mtu mwingine au karibu nao, kumbuka kuomba ruhusa kabla ya kuchukua yoyote.

Jisajili au fuata podikasti ya Australia Yafafanuliwa kwa taarifa na vidokezo muhimu zaidi kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.

Je unaswali au pendekezo la mada?

Tuma barua pepe australiaexplained@sbs.com.au


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now