Je, unajua nani anaweza kusaidia kuhusu kibali cha biashara, tatizo la upangaji nyumba, au msaada wa kifamilia? Kupitia hadithi za Fedele, Carol na Abeer, fahamu jinsi ngazi tatu za serikali nchini Australia zinavyofanya kazi. Jua majukumu ya serikali za mitaa, serikali za majimbo au maeneo ya utawala, na serikali kuu (ya shirikisho), pamoja na mahali pa kupata msaada.
Katika sehemu ya kwanza ya *How Australia Works*, Fedele anataka kuanzisha biashara, Carol anajaribu kutatua mgogoro wa upangaji, na Abeer anahitaji msaada katika kulea familia yake. Hadithi zao zinasaidia kueleza jinsi ngazi tatu za serikali nchini Australia zinavyoathiri maisha yako ya kila siku, na kwa nini kufahamu ni nani anayehusika kunaweza kukusaidia kupata msaada unaofaa.
Sikiza vipindi vyote vya mfululizo huu katika lugha yako.
Yanayo jiri baadae: Chunguza majukumu mbalimbali ya bunge, serikali (tawi la utendaji) na mahakama katika kutunga, kutekeleza na kutumia sheria za Australia, na ufahamu kinachotokea unapopinga faini.
How Australia Works inapatikana katika lugha 60. Sikiza mfululizo huu katika lugha zingine.
Credits:
How Australia Works is a podcast from SBS Audio and Australia Explained.
Host: L-FRESH The LION
Research and journalism: Gonzalo Aguirregomezcorta
Sound design, mix, original music and theme: L-FRESH The LION
Law and civics consultant: Dr Jacinta Sassine, School of Law, Western Sydney University
Artwork and design: Francisco Ortiz Lozano and Yudai Urushima
Written, created and produced by: Josipa Kosanovic
Editor, Australia Explained: Roza Germian
Head of Educational and Essential Services, SBS Audio: Janine Googan
Tunatambua Walezi wa Asili wa ardhi kote nchini Australia ambapo podikasti hii hutayarishwa na kusikilizwa. Tunatoa heshima zetu kwa Wazee wa zamani na wa sasa, na tunawatambua watu wa asili wa Aboriginal na Wakaazi wa Visiwa vya Torres Strait kama Wenyeji wa Kwanza wa bara hili.
Nyaraka za Bunge kutoka Baraza la Wawakilishi la Australia kwa hisani ya Bunge la Australia. Hakimiliki ya Jumuiya ya Madola ya Australia. Inatumika chini ya leseni ya Creative Commons, kwa kuzingatia masharti husika ya leseni.

![[JPG]_How-Australia-Works_Ep1.jpg](https://assets.sbs.com.au/dims4/default/d1d4da1/2147483647/strip/true/crop/3200x1800+0+0/resize/1280x720!/quality/90/?url=https%3A%2F%2Fsbs-au-brightspot.s3.ap-southeast-2.amazonaws.com%2Fe9%2F46%2F56cf4ff54074a36476e0bcb73e13%2Fjpg-how-australia-works-ep1.jpg&imwidth=1280)
![[JPG]_How-Australia-Works_Ep0.jpg](https://assets.sbs.com.au/dims4/default/9a0f61e/2147483647/strip/true/crop/3200x1800+0+0/resize/1280x720!/quality/90/?url=https%3A%2F%2Fsbs-au-brightspot.s3.ap-southeast-2.amazonaws.com%2F8f%2F15%2F83a000db458f9fc153fde8cde907%2Fjpg-how-australia-works-ep0.jpg&imwidth=1280)



