Upinzani wa Mseto unatishia kuzuia mabadiliko ya serikali kwa NDIS, isipokuwa serikali ya Labor iharakishe sheria ya kufunga kile kinachoitwa kodi ya mjane.
Marekebisho yaliyopendekezwa ya NDIS, yaliyokusudiwa kuokoa dola bilioni 37.8 kwa muda wa miaka minne, yalitarajiwa kupitishwa wiki hii licha ya wasiwasi mkubwa kutoka kwa watetezi.
Mtaalamu wa usalama wa mtandao anakaribisha hatua ya serikali ya shirikisho, ya kuzifanya kampuni za mitandao ya kijamii kuwajibika zaidi kwa ulaghai wa mtandaoni unaosambazwa kupitia majukwaa yao. Mdhibiti wa fedha ASIC Jumatatu Agosti 17 anasema ulaghai wa uwekezaji unaotumia video bandia za A-I za waandishi wa habari, wanasiasa na wachumi kuwavutia waathiriwa, umeongezeka kwa asilimia 182 katika mwaka uliopita, na kuwagharimu Waustralia dola milioni 7.4.
Rais Hakainde Hichilema anaongoza katika matokeo ya uchaguzi wa urais Zambia, baada ya zaidi ya nusu ya majimbo kutangaza matokeo yake. Tume ya Uchaguzi imesema Hichilema amepata kura 1,544,140, sawa na asilimia 58.87, baada ya matokeo ya majimbo 135 kati ya 226 kuhesabiwa. Mpinzani wake mkuu, Brian Mundubile amepata kura 1,030,662. Mgombea anahitaji zaidi ya asilimia 50 ya kura halali ili kushinda bila duru ya pili. Ingawa uchaguzi wa Alhamisi ulikuwa wa amani kwa kiasi kikubwa, upinzani umelalamikia vitisho, ukamataji na vurugu.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.





