SKIP TO MAIN CONTENT

Taarifa ya Habari:Serikali ya shirikisho yaendelea kukabiliana na shinikizo lakutangaza msimamo wayo kwa viwango vya uhamiaji nchini

JULIAN HILL MIGRATION AMENDMENT BILL
Assistant Minister for Citizenship Julian Hill speaks to the Migration Amendment Bill 2026 in the House or Representatives at Parliament House in Canberra, Tuesday, March 10, 2026 Source: AAP / LUKAS COCH/AAPIMAGE

Serikali ya shirikisho imekuwa chini ya shinikizo la kufafanua malengo yake kuhusu mipaka ya visa, Waziri wa Mambo ya Ndani Tony Burke akiahirisha hotuba ya Klabu ya Kitaifa ya Waandishi wa Habari mwezi Agosti ambako alitarajiwa kutangaza kupunguzwa kwa uhamiaji.


Published

By Gode Migerano

Presented by Gode Migerano

Source: SBS


Skip to podcast episode content

Serikali ya shirikisho imekuwa chini ya shinikizo la kufafanua malengo yake kuhusu mipaka ya visa, Waziri wa Mambo ya Ndani Tony Burke akiahirisha hotuba ya Klabu ya Kitaifa ya Waandishi wa Habari mwezi Agosti ambako alitarajiwa kutangaza kupunguzwa kwa uhamiaji.


Upinzani wa Victoria umevunja ahadi yake ya kuunga mkono sheria ya serikali ya kufanyia kazi kutoka nyumbani, baada yakumuunga mkono mbunge wa chama cha Shooters Fishers and Farmers kupeleka muswada huo kwa uchunguzi wa bunge. Mwanasheria Mkuu Kivuli James Newbury hapo awali alisema upinzani unaunga mkono marekebisho ya serikali, na hautapinga muswada huo ambao ungewahakikishia wafanyakazi haki ya kufanya kazi kutoka nyumbani siku mbili kwa wiki.

Kiongozi wa upinzani wa chama cha EciDe na kiongozi wa muungano wa kisiasa wa Lamuka nchini DRC, Martin Fayulu, amehoji kitendo cha Serikali kujadiliana na waasi wa AFC-M23 huko Doha lakini ikawaondoa katika orodha ya wadau wa kitaifa watakaoshiriki mazungumzo ya kitaifa yaliyotangazwa na Rais Felix Tshisekedi. Akihojiwa na redio ya umoja wa Mataofa 'RadioOkapi', Fayulu amesema njia pekee ya mazungumzo hayo kufanikiwa ni kwa wadau wote kushirikishwa.

Bofya hapo juu kwa taarifa zaidi.


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now