Nchini Kenya, ukosoaji umekuwa ukiongezeka tangu tangazo la Rais William Ruto Jumatano iliyopita. Alisema kwamba biashara ndogo ndogo zinazoendeshwa na wageni nchini Kenya lazima zifunge kuanzia Jumatatu, Septemba 7.
Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa
Tangazo hili, lililokusudiwa kuwaridhisha wafanyabiashara wa maduka wa Kenya ambao walikuwa wameandamana siku chache zilizopita dhidi ya ongezeko la kodi za uagizaji, pia limezua wasiwasi mkubwa.
Warundi, Waganda, na Watanzania wengi wanafanya kazi nchini Kenya kwenye sekta za uuzaji wa chakula, nguo, na hata ujenzi. Kutokana na mijadala na utata uliojitokeza, mamlaka husika tangu wakati huo zimejaribu kufafanua msimamo wao.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






