Je! utaendelea kufanyia kazi nyumbani au utarudi ofisini jimboni NSW?

Mwanaume afanyia kazi nyumbani akimlea mwanawe

Mwanaume afanyia kazi nyumbani akimlea mwanawe. Source: Getty/kate_sept2004

Wiki hii wakaaji wa New South Wales ambao wame pata chanjo zote za Uviko-19, walipata fursa zakujumuika pamoja na jamaa namarafiki kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya siku 100 za vizuizi vyakudhibiti usambaaji wa Uviko-19.


Hata hivyo, fursa hizo zakujumuika tena kwa walio pata chanjo kamili zimekuja na changamoto kadhaa hususan kwa baadhi ya wafanyakazi. Hoja ambayo imeibuka nikama wata endelea kufanyia kazi nyumbani, au itawabidi warejee maofisini tena baada ya muda mrefu wakufanyia kazi nyumbani.

Claude ni mmoja wa wafanyakazi wanao toa huduma katika shirika la IMS mjini Wollongong, shirika hilo huwahudumia wahamiaji na wakimbizi ndani ya jamii. Kwa muda mrefu Bw Claude na wafanyakazi wenza wamekuwa wakitolea huduma zao mtandaoni kuambatana na mwongozo wa mamlaka, ila sasa baada ya mwongozo kubadilika kwa walio pata chanjo kamili, Bw Claude na wafanyakazi wenza wamejipata katika njia panda kwa upande wa utoaji wa huduma zao nyumbani au ofisini. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bw Claude alifunguka kuhusu kitendawili hicho.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

 


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service