Wa Australia milioni kumi na saba, wame sajiliwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa shirikisho ujao.
Nchini Australia, tuna tume huru inayo simamia mfumo wa uchaguzi. Tume ya Uchaguzi ya Australia, huhakikisha kuwa raia wanao stahiki wanafursa yakusaidia kuunda serikali ya shirikisho.
Wiki hii, makala ya mwongozo wa makazi yanatoa taarifa kuhusu jinsi yakupiga kura.
Licha ya uwezekano wakutozwa faini ukifeli kupiga kura bila sababu inayo kubalika, adhabu halisi zaidi nikukosa kuchangia maoni yako, kwa hiyo daima fanya utafiti na upige kura ukiwa na taarifa kamili. Pata taarifa zaidi kuhusu jinsi yakupiga kura hapa: aec.gov.au au piga simu kwa namba hii 13 23 26.
Share






