Mamia yawa Ethiopia kutoka eneo la kaskazini mwa Tigray, wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Sudan katika siku mbili zilizopita, wakikimbia mapigano karibu na mpaka.
Mdhibiti wa ushindani [[ACCC]] ameombwa na serikali ya shirikisho kufuatilia vituo vya mafuta kwa matukio yoyote ya kuongeza bei kupita kiasi - sasa kwa kuwa punguzo la muda la ushuru wa mafuta limeisha. Mweka Hazina Jim Chalmers anasema ameiandikia ACCC, akiomba uchunguzi zaidi wa bei za mafuta ili kuhakikisha hazijaongezwa kwa njia bandia.
Mamlaka zinatarajia hasara kubwa ya wanyamapori huku homa ya ndege aina ya H-5 ikienea, baada ya vipimo vya maabara vya C-S-I-R-O kuthibitisha tukio la kwanza la vifo vya wingi vya virusi hivyo katika idadi ya ndege wa eneo hilo. Vipimo vilifanywa kwa ndege waliokufa na wanao ugua kutoka Balden Rocks karibu na Cape Jaffa Kusini mwa Australia, na kuthibitisha kwamba wote wameambukizwa homa ya ndege aina ya H-5.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






