Hata hivyo, uamuzi huo unaweza leta changamoto zakipekee haswa, kwa wahamiaji wapya na wazazi ambao wamepata mtoto wao wa kwanza.
Katika makala ya leo ya Australia yafafanuliwa, tuta jadili maswala yaki afya ambayo yanaweza ibuka unapo tumia mfumo wa huduma ya malezi ya watoto nchini Australia.
Mara nyingi wahamiaji hukosa msaada wa familia, hali ambayo huwaacha bila uwezo wakutegemea wazazi wao kuwasaidia kulea watoto wakiwa kazini.
Elimu ya mapema ya watoto inaweza kuwa mhimu katika kesi hii na, inapendekezwa nchini Australia kwa sababu inawaruhusu wazazi warejee katika nguvu kazi.
Kuwasajili watoto katika kituo cha malezi ya watoto pia ni chaguzi maarufu, kusaidia kujenga kinga miongoni mwa watoto wachanga.
Zaidi ya hiyo, elimu ya awali ya watoto huwaandaa kwa shule kijamii na kielimu.





