Jacinta Allan amejiuzulu kama Kiongozi wa Victoria, akisema ni uamuzi sahihi kwa Wa-Victoria. Tangazo hilo limekuja nusu saa tu baada ya changamoto inayotarajiwa ya uongozi katika mkutano uliopangwa wa chama cha wabunge, kuashiria kurudi kwa bunge la jimbo.
Australia na Singapore zimesaini makubaliano mapya ya kuimarisha usalama wa nishati, minyororo muhimu ya usambazaji na biashara. Itifaki mpya chini ya Mkataba wa Biashara Huria wa Singapore-Australia inahalalisha ahadi iliyotolewa na Waziri Mkuu Anthony Albanese na Waziri Mkuu Lawrence Wong mwezi Aprili.
Chama cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, kimeendelea kuituhumu serikali kwa kutumia mashtaka ya ugaidi kama njia ya kuwanyamazisha wakosoaji wake licha ya utawala kukanusha madai hayo. Katika taarifa yake mwishoni mwa juma lililopita, makamu mwenyekiti wa Chadema, John Heche, alitolea mfano mashtaka mapya ya ugaidi waliyopewa wanachama wao zaidi ya 50 pamoja na mhadhiri mmoja wa chuo kikuu, akisema lengo ni kuwatisha wapinzani.
Bofya hapo juu kwa taarifa zaidi.






