Itakuwa lazima kwa wafanyakazi wa huduma za wazee kupata chanjo za coronavirus, na kundi la wafanyakazi linalo lengwa linatarajiwa kupata dozi yao ya kwanza katikati ya Septemba.
Viongozi katika sekta hiyo, wamekaribisha uamuzi huo, kwa maneno ya onyo.
Serikali ya shirikisho itatoa dola milioni 11 kuruhusu makazi ya huduma ya wazee, kutoa malipo ya likizo kwa wafanyakazi kuchanjwa.
Kwa ushauri wa afya na misaada ambayo imewekwa kwa jibu la janga la COVID-19 katika lugha yako, tembelea tovuti hii: sbs.com.au/coronavirus
Share






