Argentina na Uhispania wanaishi ndoto ya kipekee ya Kombe la Dunia, baada yakutinga fainali ya kombe hilo. Mjini Buenos Aires na Madrid, mashabiki wanachangia jinsi walivyopitia tamthilia, hisia na sherehe.
Uingereza itakabiliana na Ufaransa katika mechi yakuamua mshindi wa tatu Jumapili, Julai 19 saa 1 asubuhi kwa masaa ya mashariki ya Australia, na Argentina itakutana na Uhispania katika fainali Jumatatu, Julai 20 saa 11 asubuhi kwa masaa ya mashariki ya Australia.
Mechi zote mbili zitaonyeshwa moja kwa moja bila malipo kwenye runinga ya SBS na mtandaoni kupitia SBS OnDemand.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.
Share






