Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari:Ombi latolewa kuharamisha matamshi ya chuki dhidi yawa Aboriginal na wakaazi wa Torres Strait

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili
Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Kuna wito wa kuharamisha matamshi ya chuki dhidi yawa Aboriginal na watu kutoka Visiwa vya Torres Strait, huku vikao vikiendelea katika uchunguzi wa ubaguzi wa rangi wa Serikali ya Shirikisho huko Darwin.


Published

Updated

By Gode Migerano

Presented by Gode Migerano

Source: SBS



Share this with family and friends


Kuna wito wa kuharamisha matamshi ya chuki dhidi yawa Aboriginal na watu kutoka Visiwa vya Torres Strait, huku vikao vikiendelea katika uchunguzi wa ubaguzi wa rangi wa Serikali ya Shirikisho huko Darwin.


Madaktari wanasema kipimo kipya cha damu kinaweza kutabiri mwanzo wa dalili za ugonjwa wa Alzheimer miaka mingi mapema. Ungonjwa huo husababisha watu kusahau. Kipimo hicho, ambacho madaktari wanasema kinaweza kuleta mabadiliko, hutafuta kile ambacho madaktari hukiita p-tau217, ambacho kinaweza kuwatahadharisha kuhusu ugonjwa huo miaka mitano hadi kumi kabla ya watu wenye afya njema kupata dalili. Hakuna dawa inayofaa ambayo hubadilisha athari za Alzheimer's.

Nchini Kenya, kukamatwa na bangi kunaweza kusababisha kifungo cha hadi miaka 10 jela. Hata hivyo, kwa Warastafari, marufuku hii ni sawa na kuharamisha moja ya mila kuu za dini yao. Jumuiya ya Rastafari ya Kenya haitoi wito wa kuhalalishwa kwa jumla kwa bangi. Inaomba msamaha kwa wafuasi wake, ikisema kwamba Katiba inalinda uhuru wao wa kuabudu kama kwa dini zingine.

Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now