Wakati idadi ya visa vya COVID-19 nchini Australia vinaendelea kuwa vichache, serikali inamipango iwapo maambukizi yataongezeka. Kwa hiyo wa Australia wanastahili kuwa na wasi wasi kuhusu janga la coronavirus?
Msemaji wa idara ya afya ame eleza shirika la habari la SBS kwamba, serikali "inajiandaa kwa kila tukio, ikijumuisha kuendelea kudhibiti au uwezekano wakuwa na janga". Msemaji huyo ameongezea kuwa, mpango wa jibu ya dharura wa sekta ya afya ya Australia umeundwa. Mlipuko wa maambukizi hayo uki ongezeka, mpango huo unasema kuwa " shinikizo kwa huduma ya afya, itakuwa kubwa zaidi".
Mpango huo unasema "mifano mbadala ya utuzanji kama kuanzisha zahanati zakutibu magonjwa kama mafua, zinaweza tumiwa kukabiliana na ongezeko ya mahitaji ya huduma ya afya".