Tafadhali kumbuka kuwa maoni yaliyotolewa hapa hayatumiki kwa hali zote za kibinafsi. Ikiwa unawasiwasi na hali yako ya viza, ni bora utafute ushauri wa kisheria haraka iwezekanavyo.
Kwa ushauri wa bure wa kisheria, wasiliana na kitengo cha Msaada wa Kisheria kupitia jimbo lako au kitongoji. Huduma ya Sheria kwa Wakimbizi na Uhamiaji or RAILS ni huduma ya bure yenye makao Queensland. Unaweza wapigia simu RAILS kwa namba (07) 3846 9300.
Pia unaweza wapigia simu Refugee Legal kwa namba (03) 9413 0100 Jumatano na Ijumaa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana kwa huduma ya bure.
Kwa msaada wa utafsiri, piga simu 13 14 50, taja lugha yako na ulizia kuunganishwa shirika lililoteuliwa.
Misaada ya dharura kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu inapatikana kwa watu wenye viza za muda mfupi. Tembelea tovuti ya shirika hilo kwa maelezo zaidi.